Kuhusu sisi AFYA KWANZA HEALTH FACILITY
AFYA KWANZA HEALTH FACILITY ni kituo cha afya cha tiba asili kinacho toa huduma kwa kutumia
miti shamba. kinachopatikana wilayani Rungwe, mji wa Kiwira.
AFYA KWANZA ni kituo cha afya cha tiba asili kilianzishwa kwa lengo la kutoa huduma bora za afya zinazomweka mgonjwa mbele,
kwa kuunganisha matibabu ya kisasa, tiba asilia, lishe bora na ushauri wa kiafya.
Tangu kuanzishwa kwake, hospitali imeendelea kuhudumia jamii kwa uaminifu, huruma na weledi,
huku ikijenga mazingira salama na rafiki kwa wagonjwa wa rika zote.
Dira Yetu (Vision)
Dhamira yetu ni kutoa huduma za afya kwa ukamilifu kwa wagonjwa wetu kwa kuzingatia mahitaji yao ya kimwili, kiakili, kijamii na kiroho, chini ya huduma ya uponyaji wa Yesu Kristo. Tunajitahidi kuwahudumia wagonjwa kwa upendo, huruma, heshima na weledi ili kuboresha afya na ustawi wao.
Dhumuni Yetu (Mission)
Kuwa hospitali inayoongoza katika utoaji wa huduma bora za afya nchini Tanzania kwa kuunganisha ubora wa matibabu, teknolojia, tiba asilia, lishe na huduma za kiroho kwa manufaa ya jamii.
Maadili Yetu (Core Values)
- Uadilifu: Kufanya kazi kwa uwazi, uaminifu na kuwajibika.
- Huruma: Kuwajali na kuwaheshimu wagonjwa wote bila ubaguzi.
- Ubora: Kutoa huduma zinazokidhi viwango vya kitaalamu.
- Ushirikiano: Kufanya kazi kwa pamoja kwa manufaa ya wagonjwa na jamii.
- Ubunifu: Kuendelea kuboresha huduma kwa kutumia maarifa na teknolojia sahihi.
- Heshima: Kuheshimu utu, faragha na haki za kila mgonjwa.