Nembo ya AFYA KWANZA Hospital

AFYA KWANZA HEALTH FACILITY

“Afya Yako Ndiyo Furaha Yetu”

Huduma Zetu

AFYA KWANZA Hospital imejikita katika kutoa huduma bora za afya kwa kutumia wataalamu wenye ujuzi, vifaa vinavyofaa na mazingira salama kwa wagonjwa. Tunatoa huduma mbalimbali zinazolenga kinga, uchunguzi, matibabu na ufuatiliaji wa afya kwa wagonjwa wa rika zote.

1. Huduma za Wagonjwa wa Nje (Outpatient Services - OPD)

Tunatoa huduma za uchunguzi wa afya, matibabu ya magonjwa ya kawaida na sugu, ushauri wa kitabibu pamoja na ufuatiliaji wa wagonjwa bila kulazwa hospitalini.

2. Huduma za Dharura (Emergency Services)

Tunatoa huduma za haraka kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura ili kuokoa maisha na kuzuia madhara makubwa ya kiafya.

3. Upasuaji Mdogo (Minor Surgery)

Huduma za kushona vidonda, kusafisha majeraha na matibabu mengine ya upasuaji mdogo.

4. Huduma za Magonjwa ya Ngozi

Uchunguzi wa kitaalamu na matibabu kamili ya matatizo na magonjwa mbalimbali ya ngozi.

5. Tiba ya Mwili (Physiotherapy)

Huduma za kurejesha uwezo na ufanya kazi wa mwili kwa wagonjwa wenye matatizo ya misuli na viungo.

6. Masaji ya Tiba (Therapeutic Massage)

Huduma maalum za masaji zinazosaidia kuboresha mzunguko wa damu na kuondoa maumivu na msongo wa mawazo.

7. Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango

Huduma za kina za ushauri na njia mbalimbali za afya ya uzazi na upangaji uzazi.

8. Matibabu ya Magonjwa Sugu

Uchunguzi, matibabu na ufuatiliaji wa karibu wa magonjwa kama vile shinikizo la damu na kisukari.

9. Ushauri Nasaha na Elimu ya Afya

Ushauri wa kiroho na kisaikolojia kuhusu VVU/UKIMWI, lishe bora na elimu ya afya kwa jamii.

10. Afya ya Kinywa na Meno

Huduma za uchunguzi, matibabu, na usafishaji wa meno bila haja ya kung’oa pale inapowezekana.

11. Huduma za Kulazwa (Inpatient Services)

Huduma na uangalizi wa kina masaa 24 kwa wagonjwa wanaohitaji kulazwa hospitalini.

Huduma Zinazotarajiwa Kuanzishwa Hivi Karibuni

Katika mwendelezo wa kuboresha huduma zetu na kukidhi mahitaji ya jamii, hivi karibuni tutaanzisha: